LICHA
ya kucheza pungufu ya mchezaji mmoja, Tanzania Prisons imefanikiwa
kupata sare ya ugenini ya kufungana 1-1 na wenyeji, Yanga SC katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Sare hiyo inaifanya Yanga SC iendelee kukamata nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Simba na Azam ambazo pia zina mechi moja moja mkononi.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Shomary Lawi wa Kigoma aliyesaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Sylvester Mwanga wa Kilimanjaro, hadi mapumziko tayari timu hizo zilikuwa zimekwishafungana mabao hayo.
Prisons
walitangulia kwa bao la Eliuter Mpepo dakika ya tisa akitumia makosa
ya mabeki wa kati wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ na Nahodha Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ waliochanganyana na kipa wao, Mcameroon, Youth
Rostande na kushindwa kuokoa.
Prisons walipata pigo dakika ya 36 baada ya mchezaji wake, Lambert Sibiyanka kutolewa kwa kadinyekundu na refa Lawi kufuatia kumpiga kiwiko beki wa Yanga, Juma Abdul.
Yanga
walitumia mwanya huo kuongeza mashambulizi kusaka bao la kusawazisha na
wakafanikiwa kupata bao dakika ya 41, lililofungwa na kiungo Raphael
Daudi aliyemalizia krosi ya mshambuliaji Ibrahim Ajib.
No comments:
Post a Comment