Mshambuliaji wa Arsenal Olivier
Giroud atakosa mechi ya Ijumaa pamoja na mechi kadhaa za wakati wa
likizo kutokana na jeraha la nyuma ya goti.
Francis Coquelin
huenda huenda akashiriki katika mechi hiyo licha ya kuguchia katika
mechi ya ushindi wa kombe la Carabao huku Shkrodan Mustafi akitarajiwa
kushirikishwa baada ya jeraha la nyonga.LIverpool nayo itamkaribisha tena Emre Can baada ya kuhudumia marufuku, lakini daniel Sturidge na Joel Matipi hawajulikani iwapo watashiriki.Alberto Moreno bado anauguza jeraha la kifundo cha mguu.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger: "unapokuwa na kazi ya ukufunzi kwa muda mrefu kuna mechi ulizoshindwa amabzo zinakuumiza roho kwa miaka maisha yako yote.
''Unapoweza kurekebisha , jaribu. Kwa hivyo wacha tugange yanjayo na kujitokeza siku ya Ijumaa na mchezo mzuri tofauti''.
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp: "sidhani kama kutakuwa na mabao mengi tena, lakini tuanenda Arsenal kucheza na kupata mengi ya tunavyoweza.
''Naju ni vigumu lakini ninaamini kwamba wakati huu linawezekana''.
No comments:
Post a Comment