• Michezo Kimataifa 1/5

    Kiungo wa kati wa Liverpool Phillipe Coutinho ni moto wa kuotea mbali katika lango la Arsenal Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud atakosa mechi ya Ijumaa pamoja na mechi kadhaa za wakati wa likizo kutokana na jeraha la nyuma ya goti.

  • Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton 2/5

    Mshauri mmoja wa mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump ,amesema kuwa mfanyibiashara huyo bilionea huenda akatumia mjadala wa Jumatatu kuzua historia ya uhusiano wa kimapenzi wa Bill Clinton.

  • Waziri wa Ulinzi amewatembelea wanajeshi wa Tanzania nchini DRC 3/4

    Ikiwa zimepita siku 16 tangu kuuawa kwa askari 14 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliokuwa kwenye oparesheni ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Husssein Mwinyi amewatembelea wanajeshi wa Tanzania waliopo nchini humo.

  • Hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro 4/4

    Kilimanjaro ni miongoni wa vilele virefu vinavyofikika duniani, ni alama kwa wageni wengi kutoka duniani kote yenye kilomita za mraba 1668 (maili za mraba 641), kaskazini mwa Tanzania, karibu na mji wa Moshi wapandaji mlima wengi wanafika katika ukingo wa Kreta kwa kutumia fimbo ya kutembelea, mavazi yanayofaa na nia thabiti.

Nafasi za Ajira Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA)


TCRA Imetangaza nafasi za Ajira kwa watu wenye viwango hivi:-
Bachelor’s Degree in Information Technology, Computer Science, Computer Engineering, business information systems, Software engineering, Software Development, or equivalent qualifications from a reputable academic institution;
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 3/1/2018.
Share:

UTAFITI: Kufuga mbwa kunapunguza kwa 36% vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo


Utafiti uliofanywa na wanasayansi nchini Sweden unaonesha kuwa watu wanaofuga mbwa hupunguza hatari ya kifo kutokana na magonjwa ya moyo.
Utafiti huo unaonesha kuwa kufuga mpya hupunguza kwa asilimia 36 hatari ya kifo kwa wenye magonjwa ya moyo hususani kwa wanaoishi peke yao.
Kwenye nyumba ambazo huishi watu wengi, mbwa huwa hawana athari hii moja kwa moja lakini huweza pia kupunguza vifo hivyo vya magonjwa ya moyo kwa asilimia 15 tofauti na watu wanaoishi peke yao wakiwa wanafuga mbwa.
Hatahivyo utafiti huu haujaeleza moja kwa moja kwanini mbwa wanaweza kusababisha manufaa haya lakini imeonesha kuwa watu wanaofuga mbwa huishi maisha ya afya zaidi ya wasiofuga mbwa.
Share:

Watu 22 wahofiwa kufa maji ziwa Tanganyika baada ya boti kugongana

Maboti katika mto huo hujaa watu kupitia kiasi na hivyobasi kuzama kufuatia mawimbi makali
Maafisa nchini Tanzania wanasema karibu watu ishirini na wawili wanahofiwa kufa maji baada ya boti kugongana katika ziwa Tanganyika mapema leo asubuhi.
Mashua moja iliyokuwa imebeba takriban watu mia moja na arubaini waliyokuwa safarini kwa shughuli ya kidini iligongana na boti iliyokuwa na watu sitini na watano.
Usafiri wa nyakati za usiku umepigwa marufuku katika ziwa Tanganyika.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Sweetbert Njewike, wanaendelea kuwatafuta watu ambao hawajaonekana waliokuwa wakisafiri na vyombo hivyo.

Rais Magufuli awaonya wanaotaka kuvunja muungano wa Tannganyika na Zanzibar
Alisema shughuli za uokoaji zinafanywa kwa pamoja na vikosi vya Polisi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wananchi.
KUlingana na gazeti la mwananchi nchini humo mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba kulikuwa na dosari zilizosababisha ajali hiyo.
Alizitaja dosari hizo kuwa ukosefu wa vifaa vya uokoaji, vya kuzima moto mbali na boti kufanya safari za usiku.
Share:

Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton

Donald Trump
Mshauri mmoja wa mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump ,amesema kuwa mfanyibiashara huyo bilionea huenda akatumia mjadala wa Jumatatu kuzua historia ya uhusiano wa kimapenzi wa Bill Clinton.
Rudy Giuliani amesema kuwa Trump na Hillary wana maswala katika maisha yao ya kibinafsi ambayo ni ya aibu.
Alikuwa akijibu hisia kali zilizojiri dhidi ya Trump baada ya madai ya kuwatusi wanawake.

Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton
Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton
Bwana Trump amepoteza uungwaji mkono wa zaidi ya viongozi 20 wa chama cha Republican ,wengi ambao wanamtaka ajiondoe katika kinyang'anyiro cha urais baada ya kuzuka kwa rekodi za muongo mmoja ambapo amekuwa akijisifu kuwatumia kimapenzi wanawake.
Share:

MAJANI YA MSTAFELI NI DAWA YA SARATANI YA TEZI DUME KILA MTU AMEKUWA AKIIZUNGUMZIA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiHl8kQbvMvfWF7PSy9UcNLYdaK_yuqZl-55iZ0ilMDklfVefZBiVCvYQZwN0wXgqB5nQdSgOpdkBaLjGNan7C_oHIUvi22ibLHl6V1OtLIkxBvsZKlhCs8DXTjCr-I5vgv1PzPe2eMyg/s1600/FB_IMG_1508411530796.jpgMAJANI YA MSTAFELI NI DAWA YA SARATANI YA TEZI DUME KILA MTU AMEKUWA AKIIZUNGUMZIA

Majani ya mti wa mstafeli yamekuwa yakitumika na watu kwenye misitu ya amazon kwa maelfu ya miaka iliyopita kutibu karibu kila ugonjwa. Ndiyo hii inaweza kuwa ni habari mpya kwako hasa kama wewe siyo mfuatiliaji wa mambo haya ya tiba asili kwa ujumla lakini sasa habari unayo.

Mti huu wa mstaferi ndiyo tiba asili pekee inazungumziwa sana na watu wote duniani kwa sasa kuhusu maajabu yake ya kutibu saratani mbalimbali ikiwemo saratani ya tezi dume.

Na hiyo yote ni kwa sababu nzuri tu  ….

Majani ya mti wa mstafeli yanaziua seli za saratani mara 10000 zaidi ya mionzi. Na jambo la ajabu zaidi ni kuwa dawa hii haizidhuru seli hata kidogo tofauti na tiba ya mionzi ambayo inaziua mpaka seli nyingine zenye afya wakati wa matibabu yake.

Yaani dawa hii ya majani ya mstafeli huziwinda seli za kansa na kuziua huku ikikuachia seli zako zenye afya bora zaidi. Kama haitoshi majani ya mstafeli yanaongeza pia idadi na uwingi wa seli zako nyeupe za damu na kuongeza kinga ya mwili kwa haraka sana.

Majani haya yamethibitika siyo kutibu saratani au kansa ya tezi dume bali na aina nyingine za saratani zaidi ya 12 ambazo ni pamoja na:

1. Saratani ya damu
2. Saratani ya matiti
3. Saratani ya mlango wa kizazi
4. Saratani ya mapafu
5. Saratani ya ini
6. Saratani ya mdomo
7. Saratani ya kwenye ulimi
8. Saratani ya kongosho
9. Saratani ya kwenye mji wa uzazi
10. Na Saratani nyingine nyingi

Majani ya mstafeli ni dawa nzuri dhidi ya bakteria na fangasi mbalimbali mwilini na hivyo ni kinga dhidi ya maambukizi ya kila namna.

Majani ya mstafeli yanatibu pia:

1. Kisukari
2. Gout (maumivu ya jongo)
3. Maumivu ya mgongo
4. Yanaongeza kinga ya mwili
5. Yanaimarisha afya ya tumbo kwa ujumla
6. Kufunga choo
7. Msongo wa mawazo (stress)
8. Yanaimarisha afya ya nywele
9. Yanaimarisha afya kwenye mfumo wa upumuwaji
10. Yanaongeza afya ya ngozi
11. Mazuri kwa afya ya moyo
12. Yanadhibiti homa na kutuliza joto la mwili

Dawa kubwa ya saratani ambayo watu wengi hawaifahamu  …

Kuna wakati namtafakari Mungu na nashindwa kupata majibu kwamba kuna wakati watu wanateseka sana lakini bila sababu yoyote maalumu zaidi ya kukosa tu maarifa.

Kile nitakushangaza kidogo hapa ni kuwa uwezo huu wa majani ya mstafeli kutibu kansa uligundulika tangu mwaka 1976 na taasisi ya saratani ya Marekani lakini matokeo yake hayajawahi kuwekwa hadharani kwa watu!

Kwanini hawakutaka kutangaza kwa watu?

Hakuna mtu anayejuwa kwa hakika sababu ni nini iliyowafanya wabaki na matokeo hayo bila kutangaza kwa watu. Hata hivyo wengi wanaamini ni kutokana na vipimo na matibabu ya ugonjwa huu kuwa ni dili kubwa kwa viwanda vya madawa na biashara kubwa kote duniani.

Sababu kuweza kutibu ugonjwa mkubwa hivyo (kwa mjibu wa maoni yao) kwa kutumia mmea rahisi hivyo kupatikana ni jambo lisilo na faida. Matatizo mengi ya binadamu chanzo chake kikuu cha matatizo hayo ni hela.

Pamoja na hayo Mungu yupo na hatatuacha watu wote tuangamie kijinga hivyo. Wachache atatuokoa tu kwa namna yoyote. Hivyo watu wengi tayari wameanza kugeuka upande huu wa pili na tayari wanaona faida zake.

Utatumiaje majani ya mstafeli kama dawa?

Namna nzuri zaidi na ili kujihakikishia unapata faida zake kwa kiwango cha juu kabisa ni kutumia juisi freshi ya majani haya. Unachohitaji ni kuwa na blenda ya umeme, maji na majani mabichi ya mstafeli. Tengeneza juisi yako tuseme majani 6 unaweza kutengeneza juisi vikombe viwili (nusu lita) na unywe kikombe kimoja (robo lita) kutwa mara kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi na cha jioni kwa mwezi mmoja mpaka miwili.

Ni dawa nzuri kwa kansa karibu zote pia inaondoa uvimbe wa aina yoyote.

Unaweza pia kutengeneza chai ukitumia majani haya, unaweza pia kukausha majani yake na utwange au usage mashineni upate unga wake lakini bado juisi freshi ndiyo itakupa matokeo mazuri zaidi.

Mimi nimekupa taarifa hizo bure na wewe endelea kupeleleza zaidi na kufanya utafiti binafsi zaidi.

Kama unahitaji juisi freshi ya majani ya mstafeli tuwasiliane WhatsApp +255769142586, juisi ya majani ya mstaferi nauza 23000 inakuwa na ujazo wa lita 5 na unaweza kutumia siku 10.

Nipo Dar Es Salaam, napatikana maeneo ya Buza Sigara Temeke, ofisi yangu inaitwa Vctoria Home Remedy, naweza pia kukuletea ulipo ndani ya Dar naweza pia kukutumia popote ulipo nje ya Dar

Kama maelezo haya yanakusaidia kwa namna yoyote unaweza kunizawadia chochote kwenye TigoPesa 0714800175 (Fadhili Paulo).
Share:

Arsenal kulipiza kisasi dhidi ya Liverpool

Kiungo wa kati wa Liverpool Phillipe Coutinho ni moto wa kuotea mbali katika lango la Arsenal
Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud atakosa mechi ya Ijumaa pamoja na mechi kadhaa za wakati wa likizo kutokana na jeraha la nyuma ya goti.
Francis Coquelin huenda huenda akashiriki katika mechi hiyo licha ya kuguchia katika mechi ya ushindi wa kombe la Carabao huku Shkrodan Mustafi akitarajiwa kushirikishwa baada ya jeraha la nyonga.
LIverpool nayo itamkaribisha tena Emre Can baada ya kuhudumia marufuku, lakini daniel Sturidge na Joel Matipi hawajulikani iwapo watashiriki.Alberto Moreno bado anauguza jeraha la kifundo cha mguu.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger: "unapokuwa na kazi ya ukufunzi kwa muda mrefu kuna mechi ulizoshindwa amabzo zinakuumiza roho kwa miaka maisha yako yote.
''Unapoweza kurekebisha , jaribu. Kwa hivyo wacha tugange yanjayo na kujitokeza siku ya Ijumaa na mchezo mzuri tofauti''.
Beki wa Arsenal Shkrodan Mustafi huenda akashiriki katika mechi hiyo baada ya kupata jeraha
Beki wa Arsenal Shkrodan Mustafi huenda akashiriki katika mechi hiyo baada ya kupata jeraha

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp: "sidhani kama kutakuwa na mabao mengi tena, lakini tuanenda Arsenal kucheza na kupata mengi ya tunavyoweza.
''Naju ni vigumu lakini ninaamini kwamba wakati huu linawezekana''.
Share:

Mkenya Victor Wanyama kurudi katika kikosi cha Tottenham

Kiungo wa kati wa Tottenham Victor Mugubi Wanyama katika mechi iliopita
Kiungo wa kati wa Tottenham Victor Wanyama amerudi katika mazoezi kufuatia jeraha la goti na huenda akarudi katika kikosi cha Pochetino kulingana na meneja huyo.
Wanyama hajaichezea Spurs tangu timu hiyo ishindwe 2-1 na Chelsea mnamo mwezi Agosti.
Pochettino ambaye kikosi chake kitacheza mechi ya ugenini dhidi ya Burnley siku ya Jumamosi , anasema kuwa Spurs imemkosa sana mkenya huyo mwenye umri wa miaka 26 msimu huu.
''Ni hisia nzuri kutoka kwake'', alisema raia huyo wa Argentina.''Tutaona ni lini atashirikishwa tena''.
''Msimu uliopita alikuwa mchezaji muhimu sana kwetu.Na msimu huu , ni kweli.Katika hali ambayo unatakikana kuwa na nguvu tumemkasa mchezaji kama huyu''.
''Itakuwa vyema iwapo haraka iwezekanavyo atashiriki tena kwa sababu ni mchezaji mzuri na muhimu sana''.
Wanyama ambaye alikosa mechi mbili pekee za ligi ya Uingereza wakati Tottenham ilipomaliza ya pili msimu uliopita alipata jereha hilo wakati wa dirisha la uhamisho lililopita.
Share:

Jeshi la Uganda ladai kuwaua waasi wa ADF DR Congo

Waasi wa ADF wanaopetekeleza opresheni zao mashariki mwa DR Congo
Jeshi la Uganda linasemekana kushambulia kambi kadhaa za waasi mashariki mwa Congo.
Kwa mjibu wa msemaji wa jeshi la UPDF, shambulio hilo lilifaulu baada ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kugawana taarifa za kijasusi.
Kwa upande wake, msemaji wa serikali ya DR Congo Richard Karemire, ameviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa, ni ukweli kwamba wanajeshi wa Uganda wamevamia maeneo ya waasi na kushambulia kambi kadhaa.
Ameongeza kusema kuwa, wanajeshi hao wa Uganda hawakuingia nchini DRC, bali walitumia ndege za kijeshi pamoja na makombora mazito mazito ya kulipua mbali.
Idadi ya waasi waliouwawa bado haijatolewa.
Waasi hao wa ADF hivi majuzi walidaiwa kupanga mashambulio dhidi ya wanajeshi walinda amani wa MONUSCO.
Share:

Korea Kaskazini: Marekani inapanga kutekeleza ''uhalifu''

Marekani imemuonya rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini kusitisha majaribio yake ya silaha
Katika siku ambayo baraza la usalama la Umoja wa mataifa linapiga kura kuidhinisha vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea kaskazini, kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong-un, amesema taifa lake linawakilisha tishio kubwa la nyuklia kwa Marekani.
Katika hotuba iliyoripotiwa na shirika la utangazaji habari nchini (KCNA) Kim amesema kuendelezwa kwa haraka kwa mpango wa nchi yake wa nyuklia kunashinikiza ushawishi muhimu katika siasa za kimataifa.
Azimio la hivi karibuni la baraza hilo la usalama katika Umoja wa mataifa linalenga kupiga marufuku usafirishaji wa bidhaa zote za mafuta kwenda Pyongyang na kuitisha kurudishwa kwa raia wa Korea Kaskazini wanaofanya kazi katika nchi za nje katika muda wa mwaka.
Korea Kaskazini imetaja nakala za kiusalama za Marekani zinazosisitiza kuhusu utumizi wa mabavu dhidi ya Pyongnyang kuwa za kihalifu, vyombo vya habari vya taifa hilo zimesema.
Wizara ya maswala ya kigeni ilimlaumu rais wa Marekani Donald Trump kwa kutaka kukandamiza ulimwengu kupitia sera yake mpya ya usalama.

Rais Trump amesema kuwa Marekani itatumia nguvu dhidi ya Pyongyang
Rais Trump amesema kuwa Marekani itatumia nguvu dhidi ya Pyongyang
Siku ya Jumatatu rais Trump alisema kuwa Washington lazima ikabiliane na changamoto inayoletwa na mpango wa kutengeza silaha wa Pyongyang.
Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Korea Kaskazini amesema kuwa mpango mpya wa Marekani kuhusu usalama hauna lolote bali mpango wa kutaka kutumia nguvu kulingana na chombo cha habari cha kitaifa KCNA.
Ameilaumu Marekani kwa kutaka kujaribu kuvuruga taifa hilo na kugeuza rasi yote ya Korea kuwa eneo litakalotawaliwa na Marekani.
Siku ya Jumatatu rais Trump alielezea kuhusu mpango huo mpya akiikosoa Korea Kaskazini kwa kufanya majaribio ya silaha za kinyuklia licha ya shutuma kutoka Marekani na Umoja wa Mataifa.
Mwezi uliopita, rais wa Marekani pia aliliweka taifa la Korea Kaskazini miongoni mwa mataifa yanayofadhili ugaidi.
Share:

Hukumu ya Lulu: Yapo mengi ya kujifunza


HUKUMU ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenda Jela miaka miwili sawa na kumaliza msiba wa marehemu Steven Kanumba, hii ina maana amezikwa tena kifikra, kwa mujibu wa mama yake mzazi Flora Mtegoa.
Haki imetendeka hukumu imetolewa ni muda mwingine wa kuangalia yale ambayo yalitokea ili iwe funzo kwetu tuliobaki uraiani na bado tumepewa nafasi ya kuishi. Mapema wiki hii, Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam ilimhukumu jela miaka miwili Lulu baada ya kumkuta na hatia kwa kumuua Kanumba, Aprili 2012.
Hili liwe funzo kwa Wanatasnia zote mbili kwa muziki wa Bongofleva na Filamu, liwe funzo kwa Wazazi pia liwe funzo kwa Serikali na kila binaadamu kwakuwa siku na saa yoyote huenda likamtokea mwingine sababu hata wao hawakutarajia.
Wasanii liwe funzo kubwa kwao, ukizingatia Lulu na Kanumba wote walikuwa wasanii wa tasnia ya filamu. Wasanii wajifunze sanaa sio chombo cha kuendeshwa kwa rushwa ya ngono, kwaajili ya kumsaidia mtu afikie malengo yake, wawe na msimamo wamsaidie mtu kama wanaweza kama hawawezi wamwache aende kutafuta rizki kwingine.
Lakini sio kutumia sanaa kumlaghai mtu kwa kumwaminisha kwamba utamtoa katika sanaa yake, kumbe ulikuwa na lengo la kumtumia kwa kuchukulia kigezo cha shida zake na umri wake.
Najua wasanii wengi watakataa kwamba hawana mahusiano na wasanii wachanga, ambao wanatamani kuigiza huku umri wao ukichini ya miaka 18 tena wengine wakiwa shuleni.
Najua watakataa kwamba wao wanamashabiki wengi wanawake, lakini kundi kubwa la mashabiki hao ni wanafunzi wa Sekondari na shule za msingi ambao wengi wanandoto za kuwa na umaarufu mkubwa kama wa Wema Sepetu, Jackline Wolper au Kajala Masanja.
Wajifunze kwa mfumo wa kesi ya Lulu ulivyokuwa ukienda, ingekuwaje kama Kanumba asingekufa? Leo ingekuwa aibu ya mwaka kwa kutembea na mtoto wa miaka 16. Na pengine katika kukwepa hilo ndio maana uhusiano wa waili hao ulikuwa wa siri, hakuna aliyefahamu mpaka baada ya tukio la kifo cha Kanumba, ndipo siri ilipofichuka kwamba wawili hao walikuwa wapenzi.
Watu wa haki zote tungewasikia, huenda hukumu ya Lulu ingekuwa yake, kwa kesi ya kubaka ambapo tunajua kabisa ni miaka mingapi angetumikia jela. Hivyo hukumu ya Lulu na kifo cha Kanumba iwe somo kwa wasanii wengine, kwakuwa makosa kama hilo linaweza kutokea kwa mwingine kwakuwa maisha hayana mfumo maalumu wa kuelekea.
Unaweza usipatwe na umauti kama ilivyokuwa kwa Kanumba, lakini ukadhalilika kwa kuingia jela miaka 30 kwa kujihusisha kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18.
Hata hivyo hatutaacha kumkumbuka Kanumba, kwakuwa msaada wake wa kuinua tasnia ya filamu ni mkubwa, ingawa kifo chake kimezua maswali mengi na mafunzo yasiyokuwa na mwisho.
Lakini pia kilichomkuta Lulu, iwe funzo kwa wazazi na walezi wenye watoto aina yake, wawe wapo kwenye filamu, muziki au wanafunzi. Mtoto anabaki kuwa mtoto na mzazi ama mlezi wake lazima azingatie misingi ya kumlea mtoto, ukuaji wa Lulu sababu ya umaarufu wake haikuwa siri ya alichokuwa akikifanya, kwani mara kwa mara alikuwa akipamba kurasa za magazeti ya udaku, mara kalewa chakari harusini, mara kakutwa kwenye kumbi za burudani.
Mtoto wa chini ya umri wa miaka 18 anafuata nini kwenye kumbi za starehe? Mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 18 anaendaje harusini peke yake na kulewa?. Lawama hizi pia ziende kwa wasanii wenzake wakubwa wakati huo ambao walikuwa wakienda nae kwenye harusi na kumuacha analewa, huku wakifahamu fika kwamba licha ya kuigiza nae, lakini huyo ni mtoto bado.
Miaka Fulani uongozi wa ukumbi wa Bilicanas uliwahi kumtoa nje Lulu, kwa madai ya kuingia klabu za usiku akiwa na umri chini ya miaka 18. Na siku chache baadae alifanya sherehe kuadhimisha siku ya kuzaliwa akidai ametimiza umri wa miaka 18, lakini kabla ya hapo aliwahi kutamba kumiliki hati ya kusafiria ya mtu mzima na ana uwezo wa kusafiri popote, lakini hakuna yeyote aliyezungumza juu ya hilo si wazazi wake waka wasanii wenzie waliomzidi umri ambao wakati huo wengi walikuwa na umri sawa na mama zake, dada zake, baba zake ama kaka zake.
Suala la kutokuwa na umri wa miaka 18, lilikuja kufichuka baada ya kifo cha Kanumba, ndipo ilipobainika kuwa alidanganya umri ili iwe rahisi kwake kufanya mambo ya kikubwa kama kwenda kwenye kumbi za burudani na mambo mengine.
“Nilikuwa kila nikienda klabu nazuiwa mlangoni, naambiwa mimi mdogo… nikafikiria nikaona ngoja nifanya ‘birthday’ kisha nitangaze nimefikisha miaka 18, lakini lengo lilikuwa nisiwekewe tena vizuizi kwenda klabu,” alisema Lulu kwenye moja ya mahojiano yake na vyombo vya habari miaka ya nyuma.
Wazazi wake walikuwa wapi wakati mtoto wao anatanagaza hadharani kuwa na miaka 18 tena kwa lengo ovu, kwanini wasingemzuia? Mzazi anayemlea mtoto wake kwa maadili ni lazima angejiuliza sababu za mtoto tena binti kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa ushahidi wake Mahakamani, siku ya kifo cha Kanumba, Lulu alikuwa anaenda ‘kujirusha’ na rafiki zake, mama yake alimruhusu vipi? Mtoto wa chini ya miaka 18 anatokaje usiku na marafiki na mzazi roho iwe tuli.
Wazazi wengi katika sanaa ya filamu na muziki, wamekuwa hawaulizi mali ambazo watoto wamekuwa wakizipata, hata kudadisi ingawa magazeti yanakuwa yanaandika ukweli. Wazazi wamekuwa kimya kwa kuamini kwamba wanakula matunda ya watoto wao, hivyo linapotokea tatizo ndipo wanaposema mwanetu alikuwa akibakwa.
Ni bora kuziba ufa hata kwa matope na miti, ili ukianguka uanguke wakati umeshahamia nyumba nyingine kuliko kuuacha kwa kusema kwa maneno ukuta usianguke mpaka nihame. Lakini pia kuna la kujifunza kwa Serikali yetu kupitia wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na michezo, kupitia kitengo chake cha Baraza la Sanaa Tanzania.
Magazeti yamekuwa yakiandika habari nyingi za wasanii kuhusiana na matendo yao ya kutoka usiku, kudanganya miaka na matukio ambayo yapo chini ya umri wao. Kwa mfano kupitia mitandao ya kijamii, baba mzazi wa mwanamitindo wa video maarufu kama Tunda, amekuwa akilalamikia baadhi ya msanii kumharibu mtoto wake.
Mzee yule aliongea mengi na magazeti mengi yaliandika kwamba mwanaye bado mwananfunzi, ila wanamuziki wanamtumia katika video zao na kumharibia maisha yake ya baadaye.
Niliwahi kumsikia mwigizaji mwingine Hanifa Daud Maarufu kama Jenifa wa Kanumba, naye miongoni mwa watu waliowahi kulalamika kwamba kuna unyanyasaji wa kijinsia katika tasnia ya filamu.
Lakini sijasikia kitengo chochote cha Serikali kinachohusiana na sanaa ambacho kikaivalia njuga habari hiyo, hata kwa kuhoji umri wa binti huyo. Labda kuweka wazi kwa baadhi ya vitu kama hivi kusaidia kesi kama hii ikitokea watu kupata majibu ya haraka, mepesi na kila mtu akapata haki stahiki kwa mujibu wa sheria.
Lakini wakisema wakae kimya basi kila msanii atakuwa akimchukua mtoto akimfundisha sanaa, akiwa mkubwa anakula matunda yake mwenyewe kwa kumfanya mpenzi wake, hapo ndipo watu watakapoacha kuwapeleka watoto wao kufanya sanaa.
Kisha tutaendelea kulalamika kwamba sanaa ya Tanzania haikuwi, ndio kwanza inakufa, mara filamu za nje zinaua filamu kumbe sisi wenyewe tunaendesha filamu ili kufanya mambo yetu.
Sina lengo la kushambulia upande wowote katika makala haya, bali nataka wadau wa sanaa, wazazi na watoto kujifunza kupitia hukumu ya Lulu. Leo Lulu amehukumiwa akiwa mtu mzima, akitoka gerezani atakuwa na maisha yake na baadae atakuwa na familia, lazima ahakikishe njia alizopita yeye watoto wake hawapiti, ajifunze malezi mazuri ya watoto wake kupitia makosa waliyofanya wazazi wake kwake mpaka leo kumkuta yaliyomkuta. Lala kwa amani Kanumba.
Share:

Sikujua tumbaku ingegeuka janga kwangu


ALIPOANZA kusokota tumbaku na kuvuta akiwa na umri wa miaka 24, Maine Mshomi aliichukulia kuwa ni kiburudisho. Hakuota abadani kwamba ‘kiburudisho’ hicho kingegeuka janga katika maisha yake.
Akiwa sasa na umri wa miaka 55, Mshomi ambaye ni mkazi wa kijiji cha Lugine wilayani Kiteto katika Mkoa wa Manyara, anakumbuka alivyokuwa akivuta misokoto ya tumbaku kati ya minne na mitano kwa siku. Tumbaku aliyokuwa akivuta alikuwa akiipata kijijini ambako inalimwa lakini si kwa ajili ya biashara bali kwa matumizi yao.
Anasema alipokuwa akienda katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu, alikuwa akivuta sigara. Wakati mwingine alipatwa na mawazo ya kuacha kutumia tumbaku hususani alipokuwa hana fedha, lakini alipopata fedha aliendelea kuvuta.
Mshomi mwenye watoto wanne, anasimulia haya yote akiwa kitandani katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, jijini Dar es Salaam. Amepimwa na kubainika kwamba anasumbuliwa na saratani ya koo.
Kabla ya kufika hospitalini hapo, alishakwenda hospitali nyingine kutafuta tiba bila mafanikio. Hospitali hizo ni Mvumi iliyopo mkoani Dodoma pamoja na KCMC ya mkoani Kilimanjaro.
Anasema amekuwa akijigharimia matibabu na sasa ameshatumia si chini ya Sh milioni 1.7. Samueli Mshomi ni ndugu yake wa karibu anayesimulia kuwa kaka yake alianza kuugua Machi mwaka huu na Ocean Road walifika Agosti mwaka huu.
“Kaka yangu amevuta tumbaku kwa muda mrefu sana, takribani kipindi cha chote ujana wake,” anasema Samueli. Anaongeza: “Tulimshauri kuacha alipoanza kuumwa japokuwa yeye mwenyewe hakuwa tayari kwa madai kwamba daktari hajamwambia kama ugonjwa wake umechangiwa na matumizi ya tumbaku.”
Hata hivyo, anasema maelezo ya daktari yalionesha moja kwa moja kuwa matumizi ya tumbaku yamechangia kwa kiasi kikubwa katika ugonjwa wa ndugu yao. Samuel anasema mpaka sasa kaka yake haamini kama tatizo lake limesababishwa na matumizi ya tumbaku akihoji kwamba mbona kuna wagonjwa wengine wanaugua saratani na hawajawahi kutumia tumbaku?
Samueli anasema ipo haja ya serikali kutoa elimu ya kutosha hasa kwa wakazi wa vijijini kuhusu madhara makubwa yanayoletwa na utumiaji wa tumbaku. Mkazi huyo wa kijiji cha Songambele anasema matumizi ya tumbaku yako juu sana kijijini kwao.
Anatamani ingewezekana, serikali izuie uzalishaji wa tumbaku kutokana na madhara yake kiafya. Wakati wa maadhimisho ya siku ya kupinga matumizi ya tumbaku Mei mwaka jana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema tafiti zinaonesha takribani watu milioni sita hupoteza maisha duniani kwmwaka kutokana na utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake.
Akielezea uhusiano wa tumbaku na saratani, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga ya Saratani katika Hospitali ya Taifa ya Ocean Road, Dk Chrispin Kahesa anasema tumbaku ina kemikali zaidi ya 200 na kati ya hizo 69 zinahusishwa na saratani.
“Saratani kwa ujumla ni mkusanyiko wa magonjwa zaidi ya 200, inategemea tu ni saratani ya eneo gani, mfano, titi, koo, shingo ya uzazi na kadhalika,” anasema. Anasema takribani saratani zote zinahusishwa na tumbaku lakini zaidi ni saratani zinazoathiri maeneo ya mfumo wa chakula.
Akifafanua kitaalamu, anasema mfumo wa chakula unaanzia kwenye kinywa ukihusisha ulimi, mdomo, njia za hewa koo na tumbo. “Kuna saratani nyingine zaidi zinaongezeka kama vile saratani za kibofu, mapafu, shingo ya kizazi na kadhalika kwa sababu hizi kemikali ukizivuta zinaingia kwenye nji ya hewa lakini zinasambaa kwenye damu hadi zinakwenda kuathiri maeneo mengine,” anasema.
Anaongeza: “Kwa hiyo tafiti zinaonesha zile saratani ambazo zinaanzia kwenye njia ya chakula na mfumo wa hewa unaohusisha pia mapafu ndizo huwaathiri wengi zaidi. Anasema athari za tumbaku siyo kwa wanaotumia kwa kuvuta pekee bali hata wanaomung’unya kama wala ugoro huathirika eneo la kinywa au njia ya chakula. Dk Kahesa anasema saratani za njia ya kinywa na chakula zinaongezeka nchini.
Anasema kwa wanaume saratani inayoongoza ni ya ngozi ikifuatiwa na ya njia ya chakula ambayo kwa kiwango kikubwa inachangiwa na matumizi ya tumbaku. Hata hivyo, anasema idadi ya wagonjwa inayoonekana hospitalini ni ndogo kwa maana upo uwezekano wa wengine kufariki bila kutambulika kutokana na kutopata fursa ya kufika katika maeneo ya tiba.
“Kwa mfano, ukienda Katavi kuna matatizo mengine ya kiafya ambayo yanaendana kabisa na matumizi ya tumbaku kama vile upungufu wa nguvu za kiume,” anasema. Anasema wengine wanaotumia tumbaku pia ni watumiaji wazuri wa vitu vingine hatarishi ikiwemo pombe.
“Tumbaku inaweza kuhamasisha matumizi ya vitu vingine lakini yenyewe kama yenyewe ni shida kuijua takwimu zake. Tunaweza kusema ni ya nne kwa sababu tumbaku imeguswa kwenye kila aina ya saratani kwa sababu ya kemikali zake kuchangia.
“Unaweza kusema asilimia 60 ya saratani inachangiwa na virusi lakini ukija kwenye tumbaku kila saratani imehusishwa na tumbaku,” anafafanua Dk Kahesa. Wakati baadhi ya watu (akiwemo Mshomi) wakijipa moyo kwa kusema ‘mbona watu wengine wanavuta sigara na hawaugui saratani, Dk Kahesa anafafanua kuwa maradhi hayo huchukua muda mrefu hadi kugundulika.
Anasema umri wa sasa wa kuishi kwa Tanzania ni miaka 62 na kipindi kilichopita ilikuwa miaka 52. Hivyo anasema wagonjwa wengi kipindi kilichopita walikuwa ni wazee wenye umri wa takribani miaka 65.
“Kwa hiyo utaona watu wengi walikuwa wanafariki kabla saratani haijatokeza. Kama wangeishi miaka 80 hadi 90 wengi wangegundulika, lakini walikuwa wanatibiwa kwa maradhi mengine kama vile TB (Kifua Kikuu).
Wengine wanasema hawaoni ugonjwa wowote lakini ukweli ni kwamba vifaa vya kugundua saratani ni vya utaalamu wa hali ya juu.” Mbali na saratani, uvutaji tumbaku/ sigara pia unachangia maradhi ya moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dk Mohamed Janabi anasema athari kubwa za matumizi ya tumbaku zinakuwa kwenye mishipa ya damu ya moyo. Anafafanua kwamba moyo umezungukwa na mishipa ya damu inayoitwa coronary arteries ambayo sigara huwa inaiharibu.
“Kwa Tanzania bado uvutaji wa sigara siyo tatizo kubwa, bado halijawa kubwa, hatuwezi kuweka sigara katika orodha ya juu. Lakini wagonjwa wetu waulizwe kuhusu sigara kwa sababu ni moja ya magonjwa ya moyo. Asilimia 60 ya mgonjwa anaumwa nini tunaipata katika historia ya mgonjwa.
“Kuna wagonjwa wa moyo hapa ambao unasikia wanavuta pakiti mbili hadi tatu kwa siku, athari yake inakuwa kubwa zaidi, kwanza nafasi yake ya kuharibu mishipa ya moyo inakuwa kubwa sana na uachaji wake unakuwa mgumu kwa sababu mtumiaji atapata kitu kinaitwa withdrawer syndrome ambazo ni nyingi kidogo,” anasema.
Hata hivyo, anasema wagonjwa wanaowahudumia hospitalini hapo kwa sababu ya uvutaji wa sigara ni wachache kulinganisha na wale ambao wanapata tatizo la mishipa ya damu kutokana na mafuta na uzito.
Hata hivyo, Dk Janabi anasema ni muhimu Tanzania kuingilia kati matatizo yatokanayo na tumbaku kabla tatizo halijawa kubwa sana. Anatoa mfano akisema zipo nchi zilizoweka udhibiti wa uvutaji wa sigara.
Mfano Australia, mtu hawezi kuvuta kwenye eneo la chuo, Uingereza huwezi kuvuta kwenye baa na wala kubandika matangazo ya sigara kama vile kwenye mashindano ya magari.
Dk Janabi anasema ndani ya sigara kuna kemikali ya nikotini ambayo ina uraibu (hali ya mwili kuzoea kitu fulani). “Ikikuzoea uachaji wake unakuwa mgumu na ndiyo maana ni muhimu vyombo vya habari vikaendelea kuelimisha watu kuepuka kuvuta sigara kwa sababu ukishaanza kuvuta uwezakano wa kuacha unakuwa mgumu,” anasema Dk Janabi.
Anasema elimu inapaswa itolewe kwa wananchi kuhusu athari za sigara na ndiyo maana kwenye paketi za sigara zimeandikwa ‘uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako’. Kwa kuzingatia athari zake, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilitunga Mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti Tumbaku (WHO FCTC).
Nchi 180, zimeridhia mkataba huo ikiwemo Tanzania iliyouridhia Aprili 2007. Chama cha Kudhibiti Tumbaku Tanzania kupitia kwa mwenyekiti wake, Lutgard Kagaruki kinasisitiza kuwa tumbaku ni janga la taifa ambalo serikali katika kupambana, inapaswa isaidie wakulima kujikita kwenye mazao mbadala na kuwapatia masoko bora na ya uhakika.
“Kwa kuepuka tumbaku, taifa litakuwa limeokoa kizazi cha sasa na kijacho dhidi ya majanga ya kiafya, kiuchumi, kijamii na kimazingira, yanayosababishwa na kilimo na matumizi ya tumbaku,” anasema Kagaruki.
Share:

Takukuru, Waziri Dk Philip Mpango waikaba koo Airtel


SIKU moja baada ya Rais John Magufuli kuagiza Kampuni ya Simu ya Airtel kurejeshwa serikalini, Waziri wa Mipango na Uchumi, Dk Philip Mpango ameitisha vikao vya mfululizo kutwa nzima jana ili kuanza kuchunguza suala hilo, kwa lengo la kupata majibu.
Katika hatua nyingine, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nayo imesema imeanza kufanya uchunguzi wa kina juu ya suala hilo ili kukamilisha agizo la Rais Magufuli juu ya upatikanaji wa majibu ya sakata la Airtel kwa wakati. Juzi Rais Magufuli alimuagiza Waziri Mpango kuifuatilia Airtel ili kujua ukweli ili umiliki wake urudi serikalini kabla ya kuisha kwa mwaka huu.
Gazeti hili jana lilifanya juhudi za kumpata Waziri Mpango ili kujua mkakati wake wa kulishughulikia suala hilo kutokana na muda mfupi aliopewa na Rais Magufuli na kubaini kuwa kwa siku nzima jana, alikuwa akiendesha vikao vilivyokuwa vinajadili suala hilo. Kupitia simu yake ya mkononi, mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake aliliambia gazeti hili kuwa Waziri Mpango, alikuwa akihudhuria vikao vinavyojadili suala la Airtel.
“Sijui una shida gani, lakini tangu asubuhi Waziri yupo katika vikao, ni vigumu kwake kuzungumza na wewe wakati huu na nafikiri hata baadaye hataweza, maana vikao hivi haviwezi kuisha mapema. “Kama unavyojua jana kuna maelekezo yaliyotolewa na Rais (Magufuli) kwake, hivyo tangu asubuhi yupo katika vikao vinavyohusu suala hilo, hivyo sina hakika kama unaweza ukapata nafasi ya kuzungumza naye kwa leo,” alisema msaidizi wake huyo.
Takukuru yaanza uchunguzi Katika hatua nyingine, gazeti hili lilimtafuta msemaji wa Takukuru, Musa Misalaba ili kujua ni kwa namna gani taasisi hiyo imeanza kulifanyia kazi suala hilo kutokana na kuonekana wazi kuwepo mazingira ya rushwa, ambapo alisema tayari wameanza kufanya uchunguzi. “Kuhusu suala la Airtel, hata sisi tumesikia agizo la Rais, lakini kama mnavyojua ni suala linalohusu uchunguzi kwa hiyo tumeanza kulishughulikia.
Wakati wowote baadaye tukiwa tayari tutawapa taarifa,” alisema. Bodi ya TTCL yajitosa Aidha, katika hatua nyingine, Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imeiomba serikali kusaidia kurejeshewa kampuni ya Airtel, kwa kuwa umiliki wake si sahihi na umejaa udanganyifu mwingi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Dk Omar Nundu, alisema hakuna ubishi kuwa Airtel ni mali ya serikali chini ya TTCL, hivyo ni muhimu wakarejeshewa wakati huu, ambao kampuni hiyo imeingia katika mapambano ya kiuchumi.
Alisema itakuwa ni usaliti, iwapo Bodi ya TTCL na uongozi wa kampuni hiyo, hawatautoa hadharani ukweli kuhusu uhalali wa Airtel, na kwamba wamejitoa sadaka kuinyanyua TTCL iweze kupeleka gawio la kutosha serikalini.
Dk Nundu aliyewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Awamu ya Nne, alisema dhuluma iliyofanywa kwa kipindi chote cha utendaji wa Airtel itawekwa wazi mbele ya Watanzania na kwamba alichokifanya Rais Magufuli ni kuchokoza na wao wako tayari kutoa ushirikiano ili kampuni hiyo iweze kurudi.
Kwa mujibu wa Nundu, kikao kilichowakutanisha viongozi mbalimbali wakiwemo wa Kampuni ya Celtel na serikali kilichofanyika Agosti 5, mwaka 2005, kilijawa na maamuzi yenye vioja yaliyoifikisha Airtel mahali ilipo sasa.
Alisema kurudishwa kwa Airtel ni vita kubwa, wanayokwenda kupambana nayo kwa sasa huku wakiamini kuwa wapo watakaopata msukosuko, lakini wanachokiamini ni kurejea kwa kampuni hiyo ya Airtel chini ya utendaji wa TTCL.
“Hasara nyingi tumeipata tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo, tumewekeza mitaji mingi, ndio maana tunasisitiza kuwa upo ushahidi kuwa ni mali ya TTCL kwa asilimia 100,” alisema Nundu. Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema uongozi wa TTCL na wafanyakazi wote, wanaiunga mkono Bodi ya TTCL kwa asilimia 100 kutokana na mkakati wake wa kusimama kidete ili kuirejesha Airtel serikalini.
Alisema TTCL imeendelea kujiendesha kwa faida, ambapo alitoa mfano wa robo ya mwaka huu iliyoishia Septemba, ambapo faida iliyopatikana kutokana na mfumo wa uendeshaji ilifikia Sh bilioni 1, huku faida kabla ya kodi ikiwa ni Sh bilioni 2.66, na faida bada ya kodi Sh bilioni 1.8, wakati kodi iliyolipwa ikikaribia Sh milioni 800.
Share:

Spika EALA aahirisha bunge kupisha maridhiano


SPIKA wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Martin Ngoga amelazimika kusitisha shughuli za Bunge hilo hadi hapo zitakapoitishwa tena baada ya wabunge wa Tanzania na Burundi kutangaza kutomtambua.
Ngoga alitangaza kusitishwa kwa shughuli za Bunge hilo jana na kusema hawezi kuruhusu likaendelea kwa hatua za kuchagua wajumbe wa kamati zake, huku nchi nne tu za Sudan Kusini, Rwanda, Kenya na Uganda zikishiriki na nchi nyingine mbili zikisusa.
"Siwezi kuendelea na bunge hili kwa sababu ya akidi kutotimia, maana hatutaweza kuchagua kamati mbalimbali kutokana na mzozo wa kutonitambua mimi kama Spika. Naahirisha Bunge hili hadi hapo mtakapotangaziwa rasmi,” alisema. Hata hivyo, wakati Spika huyo alipolazimika kuahirisha Bunge hilo, tayari wabunge walikuwa wamefanya kazi ya kuchagua Kamati ya Uongozi na ndipo baadaye Bunge likaahirishwa.
Juzi wabunge wa EALA kutoka Tanzania na Burundi, walitangaza rasmi kutomtambua na kushirikiana na Spika Ngoga kutoka Rwanda, aliyechaguliwa juzi na wabunge kutoka nchi nne, badala ya sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Akizungumza kwa niaba ya wabunge wa Tanzania, Dk Ngwaru Maghembe alisema wabunge wa mataifa hayo manne, waliendesha uchaguzi bila kuhusisha wenzao wa nchi mbili za Tanzania na Burundi wakati wanajua wanakiuka Kanuni na Sheria za Mkataba wa EAC.
Alisema wabunge wote wa Bunge hilo walipofika Arusha, walipewa fomu za kuomba kuwania nafasi ya Uspika katika Bunge hilo na ndio maana wabunge kutoka nchi tatu, ambao ni Adam Kimbisa kutoka Tanzania, Ngoga kutoka Rwanda na Leontine Nzeyimana kutoka Burundi, walichukua fomu kuwania nafasi hiyo kwa vile Kanuni zinaruhusu.
"Sheria ya Mkataba wa EAC Kifungu cha Namba 6 (c) inafafanua kuwa watafanya uchaguzi kwa maridhiano na si kufuata silabi za nchi, bali kila mtu ana haki ya kugombea nafasi hiyo kwa kila nchi," alisema.
Mbunge Dk Abdullah Makame wa Tanzania alisema Katibu wa Bunge hilo, Kenneth Maddete amekiuka Mkataba wa EAC na Kanuni za EALA na zinazotamka kuwa kutakuwa na hoja ya kupiga kura ili kumchagua Spika. “Ndiyo maana Katibu wa Bunge la EALA, Maddete alieleza kuwa wagombea watatu walikuwa wamechukua fomu kuwania nafasi hiyo ya uspika, kwa vile anajua Kanuni na sheria zilikuwa zinawapa haki ya kupigiwa kura.
"Tunahitaji jumuiya ya utashi wa kisiasa na moyo wa kuvumiliana, ndio maana tuliwasubiri wenzetu wa Kenya tukachelewa kuanza Bunge.” Alisisitiza kuwa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia ipo na itatumika katika kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo la uchaguzi wa Spika. Mwenyekiti wa wabunge kutoka Burundi, Victor Burikukiye alisema hawamtambui Spika huyo kutoka Rwanda.
Alisema watu wanaweza kutafsiri vile wanavyojua, lakini Katibu Mkuu wa EALA alitoa barua kwa wabunge watatu kuwania nafasi hiyo kwa kujua kuwa wanayo haki. "Huu ni uchaguzi gani wa nchi nne kufanya uchaguzi na tunasema hatutambui uchaguzi wa Spika uliofanyika bila ya kuwepo kwa wabunge wa Burundi," alisema.
Spika anachaguliwa kwa mzunguko na sasa hivi uspika ulikuwa ni zamu ya Burundi, Rwanda na Sudan Kusini na hii nafasi hii ilikuwa ni yetu ya Burundi, kwanini watufanyie hivi,” alisema. Mbunge kutoka Uganda, Chris Opoke alisema wabunge hao wamepoteza miezi sita bila kuanza kwa bunge, hivyo hawaoni sababu ya kuchelewa tena kuendelea na bunge hilo kwa sababu ya kukosekana kwa spika, hivyo aliunga mkono Spika huyo kuchaguliwa.
Share:

Tanzania yawa ya kwanza kutumia taasisi za fedha


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi kujenga tabia ya kujiwekea akiba ya fedha kwenye taasisi za kifedha kwa kuwa ni nguzo muhimu kwa maendeleo yao. Aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akizindua Mpango wa Pili wa Taifa Huduma Jumuishi za Fedha wa Mwaka 2018 hadi 2022.
Alisema katika Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Huduma Jumuishi wa mwaka 2014-2016, mafanikio makubwa yamepatikana ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa asilimia 86 mwaka 2017, kutoka asilimia 29 mwaka 2012 ya wananchi walio karibu na huduma za kifedha.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kifedha nchini imefikia asilimia 65 na kuifanya Tanzania kuwa ya kwanza barani Afrika na ya sita duniani kwa kuboresha mazingira ya upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi.
Ili kuhakikisha Mpango huo wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha unafanikiwa katika kuwafanya wananchi kujenga tabia ya kujiwekea akiba ya fedha, Waziri Mkuu alisema, “Tunataka kuongeza kiwango cha wananchi wanaojiwekea akiba ya fedha kupitia mifumo rasmi kutoka asilimia 43 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 60 mwaka 2022.
“Kuongeza kiwango cha wananchi kuwa karibu na huduma za kifedha katika umbali usiozidi kilomita tano kutoka asilimia 86 ya mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 90 mwaka 2022; kuongeza kiwango cha wananchi wanaotumia mara kwa mara huduma za kifedha kupitia asasi za fedha na mitandao ya simu kutoka asilimia 65 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 75 mwaka 2022.”
Malengo mengine ya Mpango huo wa Pili kwa mujibu wa Waziri Mkuu ni kuongeza kiwango cha wananchi wanaotumia huduma za bima kutoka asilimia 45 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 50 mwaka 2022, kuongeza kasi ya kuwawezesha wananchi kuwa na vitambulisho vya taifa kutoka asilimia 23 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 90 mwaka 2022.
Aidha, alisema kuwa kupitia mpango huo, serikali inataka kuongeza matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika kutoa huduma za kifedha nchini. Alisema mpango huo wa Huduma za Kifedha ni muhimu kwa kuwa utalisaidia Taifa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, kukuza uchumi wa wananchi na kupunguza umaskini. Kutokana na umuhimu wa mpango huo, Waziri Mkuu alisema serikali inasisitiza kuendelea kuwepo kwa ushirikiano imara kati ya sekta binafsi na sekta ya umma.
Alisema serikali itaendelea kuimarisha miundombinu kama vile ya umeme, kuweka mazingira wezeshi ya huduma za kifedha ili kuondoa vikwazo kwa watoaji na watumiaji wa huduma za kifedha nchini. Kwa upande mwingine, serikali imewataka wajumbe wa Baraza la Taifa la Mpango Huduma Jumuishi za Kifedha kutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali kama vile vyombo vya habari na makongamano ili wananchi wengi wajue umuhimu wa huduma za kifedha kwenye maisha yao.
Share:

Mnada Mirerani waiingizia Serikali bilioni 2


KAMPUNI ya TanzaniteOne na Shirika la Madini la Taifa (Stamico) wamefanikiwa kuuza madini yenye thamani ya Sh bilioni 1.8 katika mnada uliofanyika kwa mara ya kwanza katika kijiji cha Naisinyai kilichopo wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Kampuni ya TanzaniteOne na Stamico wameweza kuuza madini hayo kwenye mnada wa madini ulioshirikisha wanunuzi wa madini kutoka kampuni mbalimbali za madini hayo za ndani na nje ya nchi.
Awali kampuni mbili za wazawa ambazo ni Tanzanite Africa Ltd na ClassicGame Ltd walijitokeza kuuza madini hayo lakini waliyaondoa kutokana na kutoridhika na bei iliyokuwa sokoni na hatimaye Kampuni za TanzaniteOne na Stamico walifanikiwa kuuza madini hayo.
Akitangaza matokeo ya mnada huo, Kamishna wa Madini nchini, Benjamin Mchwampaka alisema kuwa jumla ya gramu 47,201. 00 za tanzanite ghafi ziliuzwa kwa dola za Marekani 820,744. 00.
Alisema kutokana na mauzo hayo serikali inatarajia kukusanya mrahaba na ada ya ukaguzi dola za Marekani 57,452.08 sawa na Sh milioni 128.8. Alisema pia Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro inatarajia kulipwa Sh milioni 5.5 kwa kodi na huduma.
Naye Naibu Waziri wa Madini, Stanislaus Nyongo alisema wanampongeza Rais John Magufuli kwa kutangaza mnada huo wa madini kufanyika mkoani Manyara ili kufungua fursa za biashara katika eneo hilo.
Pia alisisitiza kuwa suala la kudhibiti utoroshwaji wa madini hususani ya tanzanite ni mojawapo ya hatua zilizochukuliwa, ikiwemo kujengwa kwa ukuta kwa kuzunguka eneo la mgodi ya tanzanite wenye urefu wa kilomita 24.5.
Alitoa rai kwa wachimbaji wa madini kuhakikisha wanashiriki katika mnada huo mara kwa mara ili waweze kuuza madini yao ya tanzanite. Awali Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alisema kuwa kampuni 12 zinazochimba madini ya tanzanite eneo la Mirerani zinadaiwa kiasi cha Sh bilioni 3 baada ya kudiriki kukwepa kulipa kodi serikalini.
Alisisitiza kuwa serikali haitasita kuwachukuliwa hatua za kisheria wachimbaji wengine wa madini hayo ya tanzanite kwani ni lazima walipe kodi ili waweze kufanya biashara zao. Naye mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya TanzaniteOne, Hussein Gonga aliipongeza serikali kwa kuwezesha mnada huo kufanyika kwa mara ya kwanza kwenye eneo hilo na kufungua fursa ya biashara kwa wakazi wa eneo hilo.
Share:

Mwimbaji wa Muziki wa injili Rose Mhando aibukia CCM, aomba kadi


Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, mwanamziki wa nyimbo za injili nchini Rose Mhando ametumbuiza katika mkutano wa Halmashauri Kuu CCM unaoendelea mjini Dodoma, kisha kuomba kujiunga na chama hicho tawala.
Awali Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Humphrey Polepole akimkaribisha jukwaani kutumbuiza, aliwatangazia wajumbe wa mkutano kuwa Rose Mhando na kundi lake atapanda jukwaani kutumbuiza na baada ya hapo, atawasilisha ombi lake la kutaka kujiunga na chama hicho tawala.
Rose aliimba wimbo wa kusifu utendaji wa Rais John Magufuli na kibwagizo kinachomalizikia na maneno ...”tuna imani nawe.” Rose Mhando, alipomaliza shoo’ yake,wajumbe wa mkutano huo kutoka mikoa yote hapa nchini waliinua mabango yao na kumshangilia.
Share:

Mazoezi ya Ukakamavu

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro (kushoto mbele) akifanya mazoezi ya ukakamavu na askari wa kikosi cha kupambana na uhalifu mkoa wa Lindi baada ya kumaliza ukaguzi wa kikosi hicho akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani humo jana.
Share:

Ajifungua mapacha wanne Mkoani Morogoro


MWANAMKE Asha Mashaka (27), mkazi wa Msamvu B, Kata ya Kihonda Maghorofani, Manispaa ya Morogoro amejifungua kwa njia ya upasuaji watoto wanne pacha.
Kati ya watoto hao, wawili ni wa kike na wawili wa kiume ukiwa ni uzazi wake wa tatu tangu aolewe na Rajab Mkwanda (31), mkazi wa Kilosa Mbuyuni, mkoani Morogoro na hivyo kufikisha idadi ya watoto sita.
Ofisa Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Grace Mulale alisema kuwa, Asha alifanyiwa upasuaji huo Desemba 18, mwaka huu katika hospitali hiyo. Mulale alisema kuwa walimpokea Asha akiwa mjamzito na walimpomchunguza waligundua kuwa hawezi kujifungua kwa njia ya kawaida isipokuwa kwa upasuaji na walimpeleka kwenye chumba cha upasuaji ili afanyiwe upasuaji huo na madaktari.
Alisema alifanyiwa upasuaji na madaktari ambapo walipatikana watoto wanne ambao ni pacha, wawili wakiwa ni wa kike na wawili wa kume wote wakiwa na afya njema pamoja na mama yao.
Naye Muuguzi wa Wodi ya Watoto katika hospitali hiyo, Rehema Nyunguchi alisema baada ya kufanyiwa upasuaji na kupata watoto hao wanne, wote walikuwa chini ya uzito wa kilogramu mbili na kuhitajika wawekwe katika chumba maalumu cha joto ili kuwaongezea ukuaji.
Kwa upande wake mama wa watoto hao, akizungumza na gazeti hili alisema, huo ni uzazi wake wa tatu na kwamba uzao wa kwanza na wa pili alijifungua kwa njia ya kawaida mtoto mmoja mmoja na wote hao ni wa kike, lakini uzazi alioupata Desemba 18, mwaka huu ni tofauti kwani alifanyiwa upasuaji na kupata watoto wanne pacha.
Alisema kwa sasa anao watoto sita, wanne ni wa kike na wawili wa kiume na kutokana na kupata pacha hao aliwaomba wasamaria kumsaidia kifedha ili aweza kutunza watoto wake kwa vile yeye na mumewe hawana kazi inayowaingizia kipato cha kutosha ingawa ni wakulima wadogo wa kilimo cha kijikimu cha mboga.
“Ninawaomba Watanzania wenzangu wanisaidie kwa hali na mali ikiwemo fedha zitakazonisaidia kuwanunulia maziwa watoto hawa pamoja na mahitaji mengine muhimu kwani mimi na mume wangu hatuna uwezo wa kifedha wa kuwalea watoto hawa,” alisema Asha.
Aliwashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa huo kwa kutoa huduma ya haraka kwake baada ya kubaini kuwa hawezi kujifungua kwa njia ya kawaida bali ni kwa upasuaji na kupata watoto hao wakiwa salama na yenye mwenyewe.
Share:

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza upandaji miti Usiishie Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa kampeni ya kupanda na ustawishaji miti isiishie Dodoma mjini tu bali ienee katika Wilaya zote za mkoa wa huo na hatimaye nchi nzima.

Makamu wa Rais aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani.

Makamu wa Rais alisema upandaji miti si kwa ajili ya kuhifadhi mazingira tu bali ni fursa ya kiuchumi, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo alitolea mfano mti mmoja uliokomaa unaweza kunyonya hadi kiasi cha kilo 150 za gesi ya hewa ya ukaa kwa mwaka,husaidia kupunguza joto, kusaidia kuboresha afya zetu za mwili na akili kama tafiti zinavyoonyesha .

“Ni dhahiri, kampeni hii ya kuifanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma kwa vitendo.” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Wana Dodoma kuipokea kampeni hii kwa mikono miwili na kutoa kila aina ya ushirikiano ili kufikia lengo zuri lililokusudiwa.

Makamu wa Rais ambaye alihamia rasmi mjini Dodoma siku ya ijumaa tarehe 15 Desemba, 2017 alitoa pongezi kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Ofisi yake kwa kuja na wazo zuri .

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa hategemei kuona zoezi la upandaji miti lianze na kuisha leo, na badala yake liwe la kudumu, pia alizitaka manisapaa zitunge sheria ndogo zitakazoelekeza shule, chuo, taasisi na familia kuanzisha bustani ndogo za miti zitakayomudu mazingira husika,Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa ni vyema kupunguza ukataji wa miti kiholela ambapo alizitaka sheria, kanuni na taratibu zizingatiwe kabla ya kukata miti na kusema tupande miti kabla ya kukata mti.

Makamu wa Rais alimalizia kwa kutoa shukrani kwa kampuni ya TATU Mzuka kwa kujitoa na kuhakikisha kampeni hii inatekelezwa na kutoa wito kwa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania iige mfano na kuelekeza makampuni mengine ya bahati nasibu yaweze kutoa mchango wake katika shughuli za kijamii hususan kwenye suala la hifadhi ya mazingira.

Pia Makamu wa Rais alitoa shukrani kwa Jeshi la Kujenga Taifa Makotopora, DUWASA, Magereza na Tanzania Forest Services (TFS) kwa kujitoa na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hili.
 
Mwisho, Makamu wa Rais aliwataka Wanawake wa mkoa wa Dodoma kuanzisha vikundi mbali mbali vya upandaji.

Share:

Emmanuel Okwi Aitwa Baba

OKWIII
Mshambuliaji wa Simba na timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi amefanikiwa kuwa baba kwa mara nyingine, hiyo ni kutokana na mkewe kujifungua mtoto wa kike.

Mtoto huyo ambaye ni wa pili kwa Okwi na mkewe baada ya awali kuwa na mtoto wa kiume, alizaliwa jana Ijumaa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Okwi ametuma ujumbe wa furaha kwa mashabiki wake akiwajulisha juu ya kuongezeka kwa familia yake, mapema leo Jumamosi.

Okwi ameandika ujumbe huu: “Some good news to share with you fam. Yesterday we welcomed a beautiful princess into this world. Both Mum and the baby are fine. @florahwoods_mrs_okwi you are such a wonderful Mum.”
Share:

Tanzania prison yaigomea Yanga

1
LICHA ya kucheza pungufu ya mchezaji mmoja, Tanzania Prisons imefanikiwa kupata sare ya ugenini ya kufungana 1-1 na wenyeji, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Sare hiyo inaifanya Yanga SC iendelee kukamata nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Simba na Azam ambazo pia zina mechi moja moja mkononi. 

Katika mchezo huo uliochezeshwa na Shomary Lawi wa Kigoma aliyesaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Sylvester Mwanga wa Kilimanjaro, hadi mapumziko tayari timu hizo zilikuwa zimekwishafungana mabao hayo.
Prisons walitangulia kwa  bao la Eliuter Mpepo dakika ya tisa akitumia makosa ya mabeki wa kati wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ waliochanganyana na kipa wao, Mcameroon, Youth Rostande na kushindwa kuokoa.
 
Prisons walipata pigo dakika ya 36 baada ya mchezaji wake, Lambert Sibiyanka kutolewa kwa kadinyekundu na refa Lawi kufuatia kumpiga kiwiko beki wa Yanga, Juma Abdul.
Yanga walitumia mwanya huo kuongeza mashambulizi kusaka bao la kusawazisha na wakafanikiwa kupata bao dakika ya 41, lililofungwa na kiungo Raphael Daudi aliyemalizia krosi ya mshambuliaji Ibrahim Ajib. 
Share:

Popular Posts

Followers

Search This Blog

My Blog List

Labels

Contributors

Recent Posts

Pages